Friday, November 19, 2010

Siku ya mwisho ya mafunzo yetu juu ya matumizi ya intaneti.

Ni siku ya Ijumaa tarehe 19/11/2010 kama ada tunafika katika chumba cha mafunzo na kukutana na mgeni,huyu si mwengine bali ni mwandishi wa siklu nyingi hapa nchini Mwalimu MAGGID MJENGWA.
Toka siku ya kwanza tulijulishwa na wenyeji wetu MISA Tan kuwa siku ya mwisho atakuwepo huyu bwana kwa ajili ya somo la “blogg”.

Mjengwa alianza kwa kutusalimu na kisha kutupatia historia fupi ya maisha yake kwa ufupi kwa njia ya simulizi.

Hakika ni historia iliyojaa changamoto kweli na mtu wa kuigwa.
Anaanza kutuingiza katika somo na zaidi namna ya kuandika hasa kwenye mitandao na kupata mafanikio.

Ni somo gumu kiasi kwetu ambao weledi wa “computer’sio mzuri sana lakini kwa uzoefu wake anatupeleka taratibu na wengi tunapata mwanga juu ya somo.

Anatumia mifano halisi kufundisha na hili linawasaidia sana washiriki.
Mjengwa anatupa pia ujuzi wa namna ya kusoma maoni katika blogg zetu nk,pia kuhusu namna ya kuingiza picha katika blogg zetu na vitu kama hivyo.

Mwisho anatuachia ujumbe wa kujiaamini,kujitambua na kasha kuthubutu iwapo tunataka kufanikiwa maishani.

Hii ni mada ya mwisho katika mafunzo yetu kwa leo.Lakini kwa hakika kwa siku zote tano tulizokaa hapa darasani zimekuwa siku za thamani mno kwetu.
Kila tulichojifunza ni muhimu kwa mwandishi wa habari wa zama hizi za sayansi na teknolojia.

Tunawashukuru sana waandaaji MISA Tan na mwezeshaji Peik Johansson kutoka Finland.

Wito wetu kwao ni kuwa na fursa kama hizi mara nyingi na kwa waandishi tofauti wa habari kadri watakavyokuwa na uwezo na fursa ili kusaidia nchi yetu kuwa na waandishi mahiri zaidi.

Assalaam alaykum!!
ARUSHA 16/11/2010

No comments:

Post a Comment